Pablo aweka msisitizo mechi dhidi ya Red Arrows

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesisitiza kuwa katika mchezo wa kesho dhidi ya Red Arrows tunapaswa kuwa makini kutumia nafasi tutakazopata na kuimarisha ulinzi na kupunguza makosa.

Pablo amesema mchezo bado haujamalizika licha ya kuwa tuna mtaji wa mabao matatu tuliyopata kwenye mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa jijini Dar es Salaam siku chache zilizopita.

Pablo amesema anafahamu Red Arrows wataingia kwa kushambulia kwa kuwa hawana wanachohitaji zaidi ya mabao ili kufuzu hatua ya makundi hivyo amesisitiza umakini muda wote.

“Tunahitaji kuwa makini muda wote. Nafasi tukazopata tunatakiwa kuzitumia, wapinzani wataingia kwa nguvu kuhakikisha wanapata mabao, wao hawana cha kupoteza na watakuwa na faida ya kucheza nyumbani hivyo tunapaswa kuchukua tahadhari.

“Simba ni timu kubwa na ina wachezaji bora, tumejipanga vilivyo kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na kuingia hatua ya makundi ya Shirikisho Afrika,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

 1. Oh mу goodness! Awesome article dude! Τhanks,
  Howeveг I аm experiencing pr᧐blems with your RSS.
  I dоn’t know the reason ᴡhy I am unable tⲟ subscribe
  to іt. Is therе anyone eⅼse haing the same RSS issues?

  Αnyone who knowѕ the answer can you kinely respond?
  Thanx!!

  Alsο visit my ρage: uwell,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER