Pablo awapongeza wachezaji ushindi dhidi ya Pamba

Kocha Mkuu Pablo Franco, amewasifu wachezaji baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Pamba FC na kufanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Pablo amesema ilikuwa mechi nzuri ambayo tuliitawala kwa kiasi kikubwa ambayo kama tungeongeza umakini tungepata ushindi mnono zaidi.

Pablo ameongeza kuwa kipindi cha kwanza tulipoteza nafasi nyingi za kufunga lakini hakutuzitumia vizuri lakini mabadiliko tuliyofanya yalituwezesha kupata ushindi huo mnono.

“Kwanza niwapongeze wachezaji kwa ushindi huu, ni jambo jema tumefuzu nusu fainali. Mchezo ulikuwa mzuri lakini tuliokuwa na nafasi ya kupata ushindi mnono zaidi,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER