Pablo awamwagia sifa wachezaji

Kocha Mkuu Pablo Franco, amewasifu wachezaji kwa kujituma ywanjani wakati wote na kuonyesha kiwango safi uliofanikisha ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo.

Amesema kwa mara ya kwanza tangu tuanze Michuano ya Mapinduzi leo ndiyo imechezwa mechi bora kwa sababu hakukuwa na vurugu kila timu ilicheza kandanda safi.

“Kwa sasa kikosi kinaendelea kuimarika siku hadi siku na mashabiki wasubiri kuona soka safi hapo baadaye.

“Pia nimefurahi kwa jinsi wachezaji wangu walivyojituma. Walihakikisha tunapata ushindi na kuonyesha soka safi, lakini pia mchezo ulikuwa mzuri kwakua timu zote zilicheza vizuri.

“Nimefurahi pia kwa sababu mashabiki walikuja wengi na walishuhudia kandanda safi, kikosi kinaendelea kuimarika sasa tumefikia asilimia 50,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER