Pablo atua nchini

Kocha Mkuu Pablo Franco raia wa Hispania tayari ametua nchini leo kuanza kibarua cha kukinoa kikosi chetu.

Pablo 41, amepokelewa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) tayari kuanza majukumu yake wakati tukijiandaa na mchezo wetu wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting, Novemba 19.

Pablo ambaye amewahi kuwa kocha msaidizi wa Real Madrid amefurahishwa na mapokezi aliyopata na anaamini kwa pamoja tutapata mafanikio.

Kabla ya kutua Pablo kupitia video amesema amefurahi kujiunga na timu yetu kutokana na ukubwa wake barani Afrika pamoja na mashabiki wengi.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER