Pablo atoa neno kuelekea mechi dhidi ya ASEC

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema ana imani kuanzia sasa timu itaanza kufunga mabao mengi tukianza na mchezo wa kesho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas.

Pablo amesema kumekuwa na changamoto ya kupata mabao licha ya kutengeneza nafasi nyingi lakini tayari suala hilo limefanyiwa kazi mazoezini na kila kitu kiko sawa.

Akizungumzia mchezo wenyewe Pablo amesema utakuwa mgumu kutokana na ubora wa ASEC pamoja uzoefu wao lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda katika uwanja wa nyumbani.

“Ninaamini tutaanza kupata mabao mengi, tumekuwa tukifanya mazoezi sana kuhusu ufungaji na kila kitu kitakaa sawa kuanzia kesho,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER