Pablo apania kuifikia rekodi ya mwaka 1993

Kocha Mkuu Pablo Franco, ameweka wazi kuwa baada ya kupita miaka 29 tangu kufika nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika sasa muda umefika wa kuifikia rekodi hiyo.

Mwaka 1993 tulicheza fainali ya michuano hii na kupoteza mbele ya Stella Abidjan ya Ivory Coast na sasa tunataka kutinga nusu fainali kwa kuifunga Orlando Pirates kesho kisha tufike fainali.

Pablo amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na Orlando kuwa timu bora na ipo nyumbani lakini tumejipanga kuhakikisha tunapambana mpaka mwisho ili kufuzu.

Pablo ameongeza kuwa tuna faida ya bao moja tulilopata kwenye mchezo wa nyumbani kwa hiyo tutaingia kwa kutafuta jingine la mapema ili kuwachanganya Orlando.

“Imepita miaka 29 tangu tulipocheza fainali ya michuano hii. Watanzania wanatamani kuiona timu yao ikifika hatua hii na tumejipanga kuhakikisha tunapita kwa kuitoa Orlando,” amesema Pablo.

Kwa upande wake kiungo mshambuliaji, Rally Bwalya amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri morali ipo juu tayari kwa mchezo.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa mchezo, tumepokea mafunzo ya kutosha kutoka kwa walimu. Tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tutapambana hadi mwisho ili kufuzu nusu fainali,” amesema Bwalya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER