Pablo apanga kikosi kivingine

Kocha Mkuu Pablo Franco, amebadili mfumo kuelekea mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar ambapo ameamua kutotumia mshambuliaji asilia.

Katika kikosi cha leo Pablo ameamua kuwapanga viungo washambuliaji wanne Clatous Chama, Bernard Morrison, Pape Sakho na Rally Bwalya.

Morrison atatumika kama mshambuliaji bandia ‘false number nine’ huku Chama akisimama kama namba 10.

Katikati ya uwanja kutakuwa na viungo wawili wakabaji Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Pape Sakho (10), Mzamiru Yassin (19), Bernard Morrison (3), Clatous Chama (17), Rally Bwalya (8).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Hassan Dilunga (24), Medie Kagere (14), John Bocco (22), Yusuf Mhilu (27).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER