Pablo anena ushindi dhidi ya Orlando

Kocha Mkuu Pablo Franco, ameweka wazi furaha yake ya ushindi wa bao moja nyumbani tuliopata dhidi Orlando Pirates akisema unatupa faida kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo nchini Afrika Kusini.

Pablo amesema michuano ya Afrika ni migumu hivyo unapaswa kutumia vema uwanja wa nyumbani ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye mchezo wa marudiano.

Pablo ameongeza kuwa tunatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Orlando kwenye mchezo wa marudiano lakini tutajipanga kuhakikisha tunaenda kufanya vizuri ugenini.

Pablo amekiri kuwa hatukuwa na matokeo mazuri kwenye mechi za ugenini katika hatua ya makundi kwa hiyo tunapaswa kujipanga hasa kutokana na ubora wa wapinzani.

“Michuano ya Afrika mara nyingi timu zinafanya vizuri nyumbani kama tulivyofanya. Tutajipanga kuelekea mchezo wa marudiano ugenini tunahitaji kufuzu nusu fainali,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER