Pablo akiri Geita ni timu bora

Kocha Mkuu Pablo Franco ameweka wazi mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Geita Gold utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani.

Pablo amesema Geita wana timu nzuri na pia wachezaji wazuri mmoja mmoja ndiyo maana wapo katika nafasi nzuri kwenye msimamo hivyo mchezo utakuwa mgumu.

Pablo ameongeza kuwa ingawa mbio za ubingwa kwetu ni ngumu lakini tutahakikisha tunashinda kila mchezo ili kumaliza tukiwa na alama nyingi kwa ajili ya heshima ya klabu na mashabiki.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Geita inacheza kitimu pia ina wachezaji wazuri mmoja mmoja, walitupa upinzani mkubwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Bado hatujakata tamaa na ubingwa ingawa tuna nafasi finyu lakini lengo letu ni kuhakikisha tunapata alama tatu katika kila mchezo kwa ajili ya heshima ya klabu na mashabiki,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. simba kwa msimu huu tumeangushwa na ratiba ngumu tuliopangiwa but sio mwisho kuanguka ndo kujifunza next time tupambanie ubingwa nashauri safu ya ushambuliaji iboreshwe na timu ipambane kweli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER