Pablo afurahia pointi moja ugenini

Kocha Mkuu Pablo Franco, ameweka wazi furaha yake ya kupata alama moja katika mchezo wa ugenini wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendarmerie Nationale ya Niger.

Pablo amesema alama moja ugenini ina maana kubwa na imeongeza hali ya kujiamini kikosini kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Pablo ameongeza kuwa tumekuwa timu ya kwanza kupata alama moja ugenini kwenye kundi letu kwa kuwa michuano ni migumu na kila timu inajipanga kushinda nyumbani.

“Kama kocha nilitamani tupate alama tatu katika mchezo huu lakini baada ya kushindikana siyo mbay nimefurahi kupatikana kwa alama moja.

“Pointi moja ugenini ina maana kubwa kwetu, lakini pi tumekuwa timu ya kwanza katika kundi letu kufanya hivyo. Pointi moja imeongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji wetu na kuona kila kitu kinawezekana,” amesema Pablo.

Sare hiyo imetufanya kuwa vinara wa kundi D tukifikisha pointi nne baada ya kucheza mechi mbili.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

  1. Hakika vijana walipambana sana, pongezi nyingi kwa wachezaji,bench la ufundi na viongozi wote 👏👏👏

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER