Pablo afunguka kuhusu Derby ya kesho Kirumba

Kocha Mkuu Pablo Franco ameweka wazi kuwa mchezo wa kesho wa Nusu Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya watani wetu Yanga utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza utakuwa mgumu lakini ni muhimu kwetu kupata ushindi.

Pablo amesema ushindi katika mchezo wa kesho utaongeza ari kuelekea kukamilisha msimu na tutakuwa tumekaa katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa michuano hii.

Pablo ameongeza wachezaji wapo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa kesho na kila mmoja anajua anachotakiwa kukifanya akipewa nafasi ya kucheza.

“Itakuwa mechi ngumu, tupo kwenye hatua ya Nusu Fainali na ni mchezo wa Derby lazima uwe na msisimko lakini tupo tayari kwa mapambano. Tunahitaji sana kupata ushindi katika mchezo wa kesho,” amesema Pablo.

Kwa upande wake nahodha msaidizi, Shomari Kapombe amesema kwa upande wao wachezaji wamepata maandalizi ya kutosha na wapo tayari kwa mchezo wa kesho.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho. Tunajua utakuwa mgumu, tumetoka sare kwenye mechi mbili zilizopita msimu huu na kesho ni Nusu Fainali hivyo tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuingia fainali,” amesema Kapombe.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER