Pablo afunguka Hali ya kikosi

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema kikosi kipo katika hali nzuri kuelekea mchezo wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Pablo amesema morali ya wachezaji ipo juu na wanaonekana kuhitaji kujitoa kwa ajili ya kupata ushindi katika mchezo huo muhimu kwetu msimu huu.

Tangu tulivyocheza mechi yetu ya mwisho ya ligi dhidi ya Geita Gold kikosi kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Nyamagana kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo.

“Jambo zuri ni kuwa wachezaji wapo katika hali nzuri, morali ipo juu na wanafanya vizuri mazoezini. Tunahitaji kushinda mchezo wa Jumamosi ingawa tunajua utakuwa mgumu,” amesema Pablo.

Kuhusu wachezaji majeruhi Pablo amesema wote wanaendelea vizuri na matumaini ya kuwatumia kwenye mchezo wa Jumamosi ni makubwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER