Pablo abadili nyota wanane dhidi ya Polisi leo

Kocha Mkuu Pablo Franco, amefanya mabadiliko ya wachezaji wanane katika kikosi kitakachoshuka dimbani leo kuikabili Polisi Tanzania katika Uwanja wa Ushirika ukilinganisha na kile kilichoanza juzi dhidi ya Coastal Union.

Pablo amefanya mabadiliko hayo ili kuwapumzisha wachezaji kutokana na ugumu wa ratiba unaosababisha uchovu.

Mlinda mlango Beno Kakolanya amechukua nafasi ya Aishi Manula wakati mlinzi wa kushoto Gadiel Michael akimsaidia Mohamed Hussein.

Katika kikosi kilichoanza dhidi ya Coastal juzi Alhamisi, Shomari Kapombe, Pascal Wawa na Chris Mugalu ndiyo walianza na wapo kikosini leo.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30), Shomari Kapombe (12), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Pascal Wawa (6), Erasto Nyoni (18), Rally Bwalya (8), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Chris Mugalu (7), Yusuf Mhilu (27).

Wachezaji wa akiba

Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Jonas Mkude (20), Bernard Morrison (3), Clatous Chama (17), Pape Sakho (10), Jimmyson Mwanuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER