Pablo aanza na ushindi

Kocha Mkuu Pablo Franco, ameanza na ushindi katika mechi yake ya kwanza baada ya kukiwezesha kikosi chetu kutoka kifua mbele kwa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Ukiacha ushindi huo mnono Pablo ameiwezesha Simba kuonyesha kandanda safi na kuwafanya mashabiki kufurahi hasa kipindi cha kwanza.

Medie Kagere alitufungia bao la kwanza dakika ya 17 baada kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Bernard Morrison.

Kagere alitupatia tena bao la pili dakika ya 36 baada ya kumalizia mpira uliopanguliwa na mlinda mlango Mohamed Makaka kufuatia shuti kali la mguu wa kushoto na Kibu Denis.

Kibu alitupatia bao la tatu dakika ya 44 akimalizia mpira wa kisigino uliopigwa na Kagere baada ya shambulizi zuri tulilofanya langoni mwa Ruvu.

Elius Maguli aliipatia Ruvu bao lao dakika ya 70 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shaban Msala kufuatia walinzi wetu kuzembea kuondoa hatari.

Dakika ya 72 Erasto Nyoni alikosa mkwaju wa penati uliopanguliwa na mlinda mlango Makaka baada ya Kibu kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Mzamiru Yassin, Kagere, Morrison, Hassan Dilunga na Mohamed Hussein na kuwaingiza Erasto Nyoni, Pape Sakho, Duncan Nyoni, Gadiel Michael na Yusuph Mhilu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER