Oppah apiga ‘hat trick’ Simba Queens ikiichakaza Ilala

Mshambuliaji kinara Oppah Clement amefunga mabao matatu ‘hat trick’ katika ushindi wa 4-1 tuliopata dhidi ya Ilala Queens ukiwa mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League).

Oppah alifunga bao la kwanza dakika ya 11 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 23 na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa 2-0.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ambapo Koku Kipanga alitupatia bao la tatu dakika ya 53 kabla ya Oppah kumalizia la nne kwa mkwaju wa penati.

Ilala Queens walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Fatuma Hassan dakika ya 75.

Kocha Sebastian Nkoma, alifanya mabadiliko ya kuwatoa Jackline Albert na Zena Khamis na kuwaingiza Aisha Juma na Danai Bhobho.

Ushindi huo umetufanya kurejea kileleni mwa msimamo kwa kufikisha pointi tisa baada ya mechi tatu tukiwa na mabao 26.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER