Oppa kuiongoza Simba Queens mbele ya FAD FC

Mshambuliaji kinara wa timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens, Oppa Clement ataongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa leo wa kukamilisha hatua ya makundi dhidi ya FAD FC kutoka Djibouti.

Mchezo huo ambao utaanza saa saba mchana katika Uwanja wa Moi Kasarani, jijini Nairobi utakuwa ni wa pili kwa Oppa baada ya kukosa mechi ya ufunguzi kukokana kuchelewa kujiunga na wenzake kwa matatizo ya kifamilia.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Lady Doves, Oppa alicheza ingawa hakufunga kama ilivyo kawaida yake.

Ushindi katika mchezo wa leo utatufanya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa ataenda kushiriki michuano ya Afrika ambayo itafanyika nchini Misri.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

 1. Zubeda Mgunda
 2. Fatuma Issa
 3. Doto Evarist
 4. Juliet Singano
 5. Violeth Nicholaus
 6. Danai Bhobho
 7. Zena Khamis
 8. Joell Bukuru
 9. Mawete Musolo
 10. Oppa Clement
 11. Aisha Juma

Wachezaji wa akiba

 1. Gelwa Yona
 2. Janeth Shija
 3. Ruth Kipoyi
 4. Asha Djafar
 5. Shelda Boniface
 6. Koku Kipanga
 7. Maimuma Hamis
 8. Silivia Thomas
 9. Violeth Thadeo
 10. Jackline Albert
SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER