Opa akabidhiwa tuzo yake ya Januari

Mshambuliaji kinara wa Simba Queens, Opa Clement jana alikabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi Januari wa Serengeti Lite Women’s Premier League.

Opa alikabidhiwa tuzo hiyo na wadhamini Rani Sanitary Pad sambamba na kitita cha Sh 500,000 baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Fountain Gate.

Katika mwezi Januari, Opa amefunga mabao 10 katika michezo sita tuliyocheza huku akifanikiwa kufunga mabao matatu (hat trick) moja.

Opa anakuwa mchezaji wa kwanza kuchukua tuzo hiyo ambayo ni mpya na imeanza kutolewa Januari mwaka huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER