Onyango, Taddeo warejea mazoezini

Mlinzi wa kati Joash Onyango na kiungo mkabaji Taddeo Lwanga, wamerejea mazoezini baada ya hali zao kiafya kutengemaa kutokana na majeraha waliyopata kwenye mchezo wetu uliopita.

Wawili hao waligongana kichwani katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs uliopigwa Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo walishindwa kuendelea na mechi.

Katika mazoezi yanayofanyika leo jioni katika Viwanja vyetu vya Mo Simba Arena, nyota hao wapo pamoja na wenzao wakijiandaa na mchezo wa kesho wa Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Dodoma Jiji.

Daktari wa timu, Yassin Gembe amesema hali za nyota hao zinaendelea vizuri ndiyo maana ameruhusu kufanya mazoezi ingawa wanaendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

“Onyango na Taddeo wameanza mazoezi na wenzao leo hali zao zinaendelea vizuri kabisa lakini tunaendelea kuwaweka chini ya uangalizi wa madaktari ili wasipate maumivu mengine,” amesema Dk. Gembe.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER