Onyango kidedea tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki

Mlinzi wa kati Joash Onyango, amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month) baada ya kuwashinda mlinda mlango Aishi Manula na kiungo mshambuliaji Luis Miquissone.

Onyango raia wa Kenya anakuwa mchezaji wa pili kunyakua tuzo hiyo tangu ilipoanza kudhaminiwa na kampuni Februari mwaka huu, ambapo Miquissone alishinda.

Pamoja na tuzo hiyo pia Onyango atakabidhiwa fedha taslimu Sh 1,000,000 kutoka Emirate Aluminum.

Mshindi wa tuzo hiyo hupatikana baada ya Kamati Maalumu kupitisha wachezaji watano ambao wamefanya vizuri zaidi kwa mwezi husika na kuwachuja hadi watatu ambao wanaingia fainali na kupigiwa kura moja kwa moja na mashabiki kupitia Tovuti hii.

Mchanganuo wa kura zilivyopigwa:

Jumla ya Kura ni 25,719

Onyango Kura 20,288 Asilimia 79

Manula Kura 4673 Asilimia 18

Miquissone Kura 758 Asillimia 2

SHARE :
Facebook
Twitter

13 Responses

  1. Please we need Simba sc mask 😷🎭 for the coming Match.. we’re ready to buy them at any cost 🙏🙏🦁🦁🦁🔥🔥🔥 #DOorDIEseason2

  2. Tatizo apo lipo kweny sehem moja tu, ikitokea goli likaingia wavuni wat wanawez jisahau wakakuta wameshangilia na kupongezan kwa kukumbatiana nafkr CAF wametuwek kwny mtego muhimu ni kuwa makini t bac

  3. Mchezo bado haujachezwa. Ni vema kila mmoja kwa nafsi yake atimize majukumu yake ipasavyo ili kupata matokeo.
    Mpira wkt mwingine una matokeo katili. Wachezaji, benchi la ufundi na uongozi wa Simba sc kujiamini kupita kiwango au kutanguliza dharau dhidi ya As Vita, litakuwa kosa kubwa ambalo mbele kuna majuto.
    Alama 1 ni ndogo kwenye karatasi, lakini kuipata kunahitaji maandalizi thabiti ya wachezaji kuhakikisha wanapata matokeo.
    Ni rahisi kupiga mahesabu kwa kile kilicho mkononi.

  4. Big up man! great contribution to where we are, keep that consistence to the end of the champ league and more player trophies will be yours. Am insisting on simba face masks to be sold to the fans (at any cost we are ready to buy it) One Team #nguvu moja daima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER