Omari Omari ni Mnyama

Tumekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Omari Omari kutoka Mashujaa FC kwa mkataba wa miaka miwili.

Omari ni mchezaji kijana mwenye umri wa miaka 19 ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi tofauti Uwanjani.

Omari anaweza kucheza kwa ufasaha namba 8, 10, 11 na 7 na hicho ni moja ya kitu ambacho kimetuvutia kwake na kuamua kumsajili.

Omari ni kijana mwenye kipaji kikubwa na tunaamini uwezo wake utasaidia timu kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/25.

Mipango ya klabu ni kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa huku tukizingatia umri kwakuwa tunajenga timu imara ya muda mrefu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER