Okwa ni Mnyama

Klabu yetu imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo mshambuliaji Nelson Okwa (28) kutoka Rivers United ya Nigeria kwa mkataba wa miaka miwili.

Okwa ambaye anatumia mguu wa kushoto anaweza kucheza nafasi zote kwenye ushambuliaji na kwa ufanisi mkubwa.

Msimu uliopita Okwa ambaye alikuwa Rivers alifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mengine manne.

Okwa pia ameichezea Goround FC akiwa nahodha ambapo msimu wake wa mwisho mwaka 2019 alifunga mabao nane na kusaidia kupatikana kwa mengine matano.

Awali alipojiunga na klabu yetu Okwa alitakiwa kujiunga na wenzake katika kambi ya maandalizi nchini Misri lakini suala la vibali lilishababisha kushindikana kwa hatua hiyo.

Okwa anaungana na Moses Phiri, Augustine Okrah, Victor Akpan, Habib Kyombo, Nassor Kapama na Mohamed Ouattara ambao tumewasajili msimu huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER