Okrah fiti kuivaa Ihefu Ijumaa

Kiungo mshambuliaji, Augustine Okrah amepona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua na sasa yupo tayari kurejea uwanjani Ijumaa katika mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Ihefu FC.

Okrah alivunjika kidole cha mguu katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Februari 5.

Okrah ameanza mazoezi kamili jana na wachezaji wenzake na ameingia kambini tayari kujiandaa na mchezo wa Ijumaa dhidi ya Ihefu.

Kwa mujibu wa Daktari wa timu, Edwin Kagabo, Okrah yupo tayari kuanza kucheza mechi za kimashindano hivyo ni juu ya benchi la ufundi kumtumia.

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER