Okrah atupia tukipata sare na Ismailia

Kiungo mshambuliaji Augustine Okrah amefungua akaunti ya mabao baada ya kutupia katika mchezo wa kirafiki wa kimazoezi dhidi ya Ismailia inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri na kumalizika kwa sare ya bao moja.

Mchezo huo wa kirafiki ambao ulikuwa wa kuvutia huku timu zote zikionyesha uwezo mkubwa umepigwa katika Uwanja wa Ismailia saa 11:00 jioni kwa saa Misri ambapo huko nyumbani ni saa 12:00 Jioni.

Mechi hiyo ilikuwa ya mazoezi (Training match) ambayo ni pendekezo la Mwalimu Zoran Maki kuendelea kukiandaa kikosi chake kuelekea msimu mpya wa ligi.

Kikosi chetu kilichoanza leo ni

Beno Kakolanga
Shomari Kapombe
Gadiel Michael
Erasto Nyoni
Joash Onyango
Jonas Mkude
Augustine Okrah
Cleutus Chama
Habib Kyombo
John Bocco
Pape Sakho

Kocha Zoran alifanya mabadiliko ya kuwatoa Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Clatous Chama, Habib Kyombo, John Bocco na Pape Sakho na kuwaingiza Ally Salim, Israel Patrick, Victor Akpan, Medie Kagere, Chris Mugalu na Jimmyson Mwanuke.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER