Nyota wetu wote sita wameshuka dimbani Leo kusaidia mataifa yao AFCON

Katika michuano ya AFCON inayoendelea nchini Ivory Coast kikosi chetu kimefanikiwa kutoa wachezaji sita kutoka mataifa matatu.

Wachezaji wote leo wameshuka dimbani kusaidia mataifa yao na wamejitahidi kufanya vizuri.

Henock Inonga aliisaidia DR Congo kupata sare ya kufungana bao moja dhidi ya Morocco huku akicheza dakika 45 kufuatia kupata majeraha kichwani.

Mlinda mlango Aishi Manula, Mohamed Hussein, Mzamiru Yassin na Kibu Denis waliisaidia timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kupata sare dhidi ya Zambia katika mchezo ambao tulitawala sehemu kubwa.

Kibu pekee ndiye hakumaliza mechi baada ya kutolewa dakika ya 69 wakati Clatous Chama akiingia dakika ya 75 na kupiga mpira wa kona dakika ya 88 uliozaa bao la kusawazisha la Zambia.

Tunaendelea kuwapongeza nyota wetu kwa kazi kubwa wanayoendelea na kupigania mataifa yao kwenye michuano hii ya AFCON.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER