Nyota wetu wa Stars kurejea mazoezini leo

Wachezaji wetu sita waliokuwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kilichocheza mechi mbili za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Benin leo wanarejea mazoezini kuungana na wenzao.

Nyota hao wataongozwa na Nahodha John Bocco, mlinda mlango, Aishi Manula na Mohamed Hussein, Israel Patrick, Kennedy Juma na Kibu Denis.

Wachezaji hao wametua nchini jana alfajiri kutoka Benin walipoisaidia Taifa Stars kupata ushindi wa bao moja ugenini ambao umetufanya kuongoza kundi J.

Katika mchezo huo wachezaji wetu watano kati ya sita walianza moja kwa moja kikosi cha kwanza huku nahodha Bocco akiwa benchi.

Kikosi chetu kinajiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana ugenini utakaopigwa Jumapili, Oktoba 17.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER