Nyota wetu tisa waitwa Stars

Wachezaji tisa katika kikosi chetu wameitwa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa ajili ya mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia ambazo zitafanyika mwakani nchini Qatar.

Stars inajiandaa na mechi mbili za kufuzu fainali hizo dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Madagascar.

Nyota hao walioitwa ni mlinda mlango Aishi Manula walinzi Shomari Kapombe, Israel Patrick, Mohamed Hussein na Kennedy Juma.

Wengine ni Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin na washambuliaji John Bocco na Kibu Denis.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER