Nyota wetu saba wawakilisha mataifa yao kufuzu Kombe la Dunia

Wachezaji wetu saba wameanza kikosi cha kwanza kwenye timu zao za taifa zilizokuwa zikitafuta tiketi ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia ambalo litafanyika nchini Qatar mwakani.

Katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) kilichoibuka na ushindi wa bao moja ugenini dhidi ya Benin wachezaji watano walianza huku Nahodha John Bocco akiwa benchi.

Nyota walioanza kwenye kikosi cha Stars ni mlinda mlango Aishi Manula, walinzi Israel Patrick, Mohamed Hussein, Kennedy Juma na mshambuliaji Kibu Denis.

Katika mchezo huo Aishi ameonyesha uimara mkubwa na kuondoa michomo mingi ambayo ingeweza kuleta madhara langoni mwa Stars.

Kiungo Taddeo Lwanga ameiongoza Uganda kupata ushindi wa bao moja mbele ya Rwanda iliyokuwa inaongozwa na Medie Kagere.

Mlinzi Joash Onyango alikuwa benchi wakati Kenya ikipoteza kwa bao moja nyumbani dhidi ya Mali.

Muda mfupi ujao nyota wetu Duncan Nyoni na Peter Banda wataiwakilisha Malawi dhidi ya Ivory Coast wakati Rally Bwalya akiwa na kikosi cha Zambia kitakachoivaa Equatorial Guinea.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER