Nyota watano waliocheza dakika nyingi NBCPL

Ligi Kuu ya NBC imesimama kwa takribani wiki tatu kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoanza leo Visiwani Zanzibar.

Wakati Ligi ikiwa imesimama tayari tumecheza mechi 10 tukishinda mechi saba tukitoka sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.

Wakati tunaanza msimu tulikuwa na kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ lakini hadi ligi inasimama kupisha michuano hiyo timu ipo kwenye mikono salama ya kocha Abdelhak Benchikha.

Katika mechi hizo kuna wachezaji ambao wamecheza dakika nyingi kuliko wengine.

Makala hii inakuletea wachezaji watano ambao wamecheza dakika nyingi zaidi

1. Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’

Mlinzi wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ ambaye ni nahodha msaidizi ndiye amecheza dakika nyingi kuliko mchezaji yoyote.

Zimbwe Jr amecheza dakika 900 ambazo ni sawa na kucheza mechi zote 10 kwa dakika 90 bila kufanyiwa mabadiliko.

Katika michezo hiyo Zimbwe amecheza kwa uwezo mkubwa huku akisaidia kupatikana kwa mabao matatu (assist).

2. Che Fondoh Malone

Mlinzi mpya wa kati, Che Fondoh Malone anashika nafasi ya pili akiwa amecheza dakika 891.

Raia huyo wa Cameroon amekuwa muhimili mkubwa kwenye kikosi chetu huku akitengeneza maelewano mazuri na mlinzi Henock Inonga.

3. Shomari Kapombe

Mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji waandamizi kikosini ambaye kiwango chake hakijawahi kuwa na shaka

Kapombe ni muhimili wa timu yetu upande wa kulia na amekuwa akitengeneza mabao mengi ya kufunga pamoja na nafasi kutokana na ubora wake.

Katika mechi 10 tulizocheza mpaka sasa, Kapombe amesaidia kupatikana kwa mabao matatu (assist).

4. Fabrice Ngoma

Kiungo mkabaji, Fabrice Ngoma wala haitaji maelezo mengi kuelezea uwezo wake uwanjani.

Ngoma ameingia kwenye kikosi moja kwa moja na anashika nafasi ya nne kwenye orodha ya wachezaji waliocheza dakika nyingi akiwa amecheza dakika 885.

Katika mechi hizo Ngoma amefanikiwa kufunga bao moja akiwa hatoa assist yoyote.

5. Saido Ntibazonkiza

Kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza anakamikisha idadi ya wachezaji watano waliocheza dakika nyingi mpaka sasa ligi ikiwa imesimama.

Ntibazonkiza ambaye ni mfungaji bora wa msimu uliopita amecheza dakika akiwa amefunga mabao manne huku akisaidia kupatikana kwa jingine moja.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER