Nyota watakaotuwakilisha dhidi ya Ruvu Shooting

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Ruvu Shooting kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) utakaoanza saa moja usiku.

Baada ya kuonyesha kiwango safi katika mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas Nahodha John Bocco amepangwa kuongoza mashambulizi.

Bocco atapata msaada wa karibu kutoka kwa Clatous Chama pamoja na mawinga Yusuf Mhilu na Peter Banda.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Gadiel Michael (2), Henock Inonga (29), Pascal Wawa (6), Jonas Mkude (20), Yusuf Mhilu (27), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Clatous Chama (17), Peter Banda (11).

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Erasto Nyoni (18), Bernard Morrison (3), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14) Jimmyson Mwinuke (21)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER