Nyota watakaotuwakilisha dhidi ya Azam leo

Kocha Mkuu Pablo Franco, amefanya mabadiliko ya wachezaji watano katika kikosi kitakachoshuka dimbani leo kuikabili Azam FC ukilinganisha na kile kilichoanza na Pamba FC siku ya Jumamosi.

Katika mchezo uliopita wa robo fainali ya FA, Pablo aliwaanzisha, Jimmyson Mwanuke, Kennedy Juma, Pascal Wawa, Peter Banda na Yusuf Mhilu ambao wote wapo benchi leo.

Henock Inonga na Joash Onyango watasimama kama walinzi wa kati huku Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin wakicheza katika idara ya kiungo wa ulinzi.

Nahodha, John Bocco ataendelea kuongoza safu ya ushambuliaji akipata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji watatu Kibu Denis, Pape Sakho na Rally Bwalya.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Kibu Denis (38), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Rally Bwalya (8), Pape Sakho (10).

Wachezaji wa akiba

Beno Kakolanya (30), Jimmyson Mwanuke (21), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Taddeo Lwanga (4), Peter Banda (11), Medie Kagere (14), Yusuf Mhilu (27)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER