Nyota watakaotuwakilisha dhidi ya ASEC leo

Kikosi chetu leo kitatupa karata yake ya kwanza katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi kwa kuikabili ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Medie Kagere amepangwa kuongoza mashambulizi akitegemea kupata msaada wa karibu kutoka Rally Bwalya ambaye atacheza namba 10.

Winga Peter Banda ambaye alikuwa kwenye kikosi cha Timu yake ya Taifa ya Malawi katika Michuano ya AFCON amepangwa winga wa kulia na utakuwa mchezo wa kwanza tangu arudi nchini wakati kushoto atakuwepo Pape Sakho.

Katika kiungo wa ulinzi Kocha Pablo Franco amewapanga Jonas Mkude na Sadio Kanoute wakati Joash Onyango na Henock Inonga wakisimama kama walinzi wa kati.

Kikosi Kamili kilivyopangawa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Peter Banda (11), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14), Rally Bwalya (8), Pape Sakho (10)

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Pascal Wawa (6), Erasto Nyoni (18), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Yusuf Mhilu (27), Jimmyson Mwinuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER