Nyota wanne waliokipiga dakika 180

Tukiwa tumeanza Msimu Mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2023/24, mpaka sasa tumecheza mechi mbili na kushinda zote.

Mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar (2-4) na wa pili dhidi ya Dodoma Jiji (2-0).

Katika michezo hiyo, ni wachezaji wanne pekee ambao wamecheza mechi zote kwa dakika 90 yaani sawa na dakika 180.

Nyota hao ni mlinda mlango Ally Salim, walinzi Shomari Kapombe na Mohamed Hussein na kiungo mkabaji Fabrice Ngoma.

Nyota hawa wote wameshiriki moja kwa moja katika mabao hayo sita tuliyofunga.

Ally Salim

Mlinda mlango kijana, Ally Salim amecheza mechi zote mbili sawa na dakika 180.

Katika mechi hizo moja ametoka bila kuruhusu nyavu zake kuguswa (clean sheet) dhidi ya Dodoma Jiji.

Shomari Kapombe

Mlinzi wa kulia ambaye amekuwa kwenye kiwango bora kwa muda mrefu. Kama asipokuwa majeruhi anakuwa kwenye ubora ule ule katika kila mchezo.

Amecheza dakika zote 180 na amesaidia kupatikana bao moja lililofungwa na Moses Phiri katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.

Zimbwe Jr

Nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ hahitaji maneno mengi kumuelezea. Anamwagika jasho muda wote anapokuwa uwanjani.

Naye pia amecheza dakika zote 180 kwa ubora mkubwa akisaidia kupatikana kwa bao moja lililofungwa na Jean Baleke katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.

Fabrice Ngoma

Kiungo mkabaji mpya, Fabrice Ngoma ameanza vizuri maisha yake ndani ya kikosi chetu.

Fabrice amekuwa mchezaji muhimu wa kutuliza timu inaposhambuliwa na kuanzisha mashambulizi pamoja na uwezo mkubwa wa kufunga.

Fabrice amecheza dakika zote 180 akifunga bao moja kwa kichwa katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar akimalizia pasi ya Jean Baleke.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER