Nyota Simba Queens afunguka kuelekea msimu mpya

Kiungo mshambuliaji wa Simba Queens, Joelle Bukulu amefunguka kuwa maandalizi kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) yanaendelea vizuri na tupo tayari kutetea taji letu.

Simba Queens imepangwa kuanza kutetea ubingwa wa ligi kwa kucheza dhidi ya Ruvuma Queens mchezo utakaopigwa Desemba, 23 katika Uwanja wa Mo Simba Arena.

Bukulu amesema anaamini msimu utakuwa mgumu kutokana na timu nyingi kujiandaa vizuri lakini nasi tutahakikisha tunapambana kutetea ubingwa.

“Msimu utakuwa mgumu kwa sababu timu zote zimejipanga ili kufanya vizuri, sisi kama mabingwa tutapambana kuhakikisha tunatwaa tena taji hili ingawa tunajua haitakuwa kazi rahisi.

“Kuelekea mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Ruvuma maandalizi yanaendelea vizuri, wachezaji tupo kwenye hali nzuri tunatarajia mechi ya ushindani lakini tumejipanga kushinda,” amesema Bukulu.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. Hello just wanted to give you a quick heads up. The words
    in your content seem to be running off the screen in Firefox.
    I’m not sure if this is a format issue or something to do with browser compatibility but I thought I’d post to let you know.
    The design and style look great though! Hope you
    get the problem fixed soon. Thanks

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER