Nyota saba waitwa timu zao za Taifa

Wachezaji wetu saba wameitwa katika timu zao kwa ajili ya kujiandaa na mechi za kufuzu Kombe la Dunia mapema mwezi ujao.

Nyota watano wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ilinayojiandaa na mchezo dhidi ya Zambia wakati wawili ni kutoka mataifa ya nje.

Nyota walioitwa katika kikosi cha Taifa Stars ni mlinda mlango Ally Salim, walinzi Israel Patrick na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Wengine ni washambuliaji Edwin Balua na Kibu Denis.

Kwa upande wa wachezaji wa Kimataifa walioitwa kwenye timu zao za Taifa ni Henock Inonga (DR Congo) na Sadio Kanoute wa (Mali).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER