Nyota saba kiimataifa waitwa timu zao za taifa

Nyota wetu saba wa kimataifa wataondoka kesho kwenda kujiunga na timu zao za taifa zinazojiandaa na mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia.

Mechi za kwanza zitapigwa Oktoba 7 wakati za marudiano zitakuwa Oktoba 10 baada ya hapo wachezaji watarejea kikosini.

Mshambuliaji Medie Kagere ameitwa kwenye timu yake ya taifa ya Rwanda itakayokutana na Uganda ambayo Taddeo Lwanga naye yupo kikosini.

Peter Banda na Duncan Nyoni wameitwa kwenye Timu ya Taifa ya Malawi ‘The Flames’ ambayo inajiandaa na mchezo dhidi Ivory Coast.

Joash Onyango atakuwa na timu yake ya taifa ya Kenya ambayo itacheza na Mali.

Kiungo fundi Rally Bwalya amejumuishwa kwenye kikosi cha Zambia kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Afrika ya Kati.

Mlinzi Henock Inonga Baka pia ameitwa kwenye Tmu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo itacheza na Madagascar.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER