Nyota 26 kuondoka mchana kuelekea Zanzibar

Kikosi cha wachezaji 26 benchi la ufundi pamoja na Viongozi kitaondoka saa sita mchana kuelekea Zanzibar tayari kwa kushiriki michuano ya Muungano.

Michuano ya Muungano imerejea baada ya kupita miaka 20 ambapo sasa itashirikisha timu nne, mbili kutoka Tanzania Bara na nyingine mbili kutoka Zanzibar.

Sisi tumepangwa kucheza na KVZ katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza itakayopigwa kesho saa 2:15 usiku katika Uwanja wa New Amaan Complex.

Mshindi wa mchezo wetu atakutana na mshindi kati ya Azam FC dhidi ya KMKM ambao watakutana Alhamisi saa 2:15 katika dimba hilo hilo la New Amaan Complex.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER