Kikosi cha wachezaji 23 kimeondoka jijini Dar es Salaam mchana kuelekea Zambia tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos.
Kikosi kimeondoka na benchi zima la ufundi likiongozwa na kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’.
Baada ya kufika Zambia kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho kesho jioni katika Uwanja wa Levy Mwanawasa ambao tutautumia kwa mchezo wetu wa Jumamosi.
Tunaondoka huku tukijua tunaenda kwenye mchezo mgumu na tunaiheshimu Power Dynamos lakini tumejipanga kufanya vizuri.
Tutaingia kwenye mchezo tukiwa na lengo moja la kutafuta ushindi kwenye mchezo wa ugenini ili kujiweka kwenye mazingira mazuri katika mechi ya mkondo wa pili.