Ntibazonkiza ni Mnyama

Uongozi wa klabu unatangaza kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo mshambuliaji Saidi Ntibazonkiza kutoka Geita Gold Fc kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

Ntibazonkiza raia wa Burundi ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa akiwa amecheza ligi za mataifa mbalimbali ikiwemo Ufaransa, Uturuki, Poland na hapa nyumbani ameshacheza ligi ya Tanzania kwa zaidi ya misimu miwili akiwa na timu mbalimbali.

Kwa uzoefu wa Ntibanzonkiza tunaamini ataongeza ubunifu katika safu yetu ya ushambuliaji akishirikiana na wachezaji waliopo.

Kwa msimu huu Ntibazonkiza amefunga mabao manne na assist Sita katika timu yake ya Geita Gold Fc

Tayari mchezaji huyo amewashawasili Jijini Mwanza kwa ajili ya kujiunga na kikosi kinachojiandaa na mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa Desemba 26 katika Uwanja wa CCM Kirumba

Saido Ntibazonkiza anakuwa ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa katika dirisha hili dogo la usajili kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi chetu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Again’ ameweka wazi safari hii tutafanya usajili makini bila shinikizo kutoka mahali popote.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER