Kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza ameshinda tuzo ya mfungaji bora wa Ligi ya NBC msimu 2022/23 baada ya kufunga mabao 17.
Ntibazonkiza amefunga mabao sawa na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ambaye nae amekabidhiwa kiatu cha dhahabu.
Katika msimu wa 2022/23 Ntibazonkiza amefunga mabao hayo 17 pamoja na kusaidia kupatikana kwa mengine 12.
Ntibazonkiza amefunga mabao hayo akiwa na timu mbili za Simba na Geita ambapo akiwa kwetu ametupia 11.