Ntibazonkiza Mchezaji bora wa mashabiki Januari

 

Kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Januari (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Saido ambaye amejiunga na kikosi chetu katika dirisha dogo Desemba amewapiku walinzi Mohamed Hussein na Shomari Kapombe.

Katika mwezi Januari, Saido amecheza mechi tatu sawa na dakika 270 akifunga mabao mawili na kusaidia kupatikana kwa lingine moja.

Mchanganuo wa kura zilivyopigwa

Kura Asilimia Nafasi

Zimbwe Jr 968 31.58 2

Kapombe 836 27.28 3

Ntibazonkiza 1261 41.14 1

Saido atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile kama sehemu ya zawadi ya kuibuka mshindi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER