Kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kiungwana (Fair Play) katika hafla ya tuzo za TFF zinazofanyika jijini Tanga.
Ntibazonkiza ameipata tuzo hiyo baada ya kuwapiku Pape Sakho na Jean Baleke aliokuwa akishindana nao kwenye kinyang’anyiro hicho.
Ntibazonkiza ameshinda tuzo hiyo baada ya kumzuia mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kwenda kumrudishia Mzamiru Yassin aliyekuwa amemfanyia madhambi katika mchezo wa Derby ya Karikakoo uliofanyika Aprili 16.