Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza tutacheza dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 8 saa moja usiku.
Mfumo huu wa kucheza Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii ni mara ya pili kutumika ambapo ulianza mwaka jana na tuliibuka Mabingwa kwa kuifunga Yanga katika mechi ya Fainali.
Mshindi wa mechi yetu atakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Azam FC dhidi ya Coastal Union.
Kikosi chetu kinaendelea kupiga kambi nchini Misri kujiandaa na msimu mpya wa mashindano na kitarejea nchini mwishoni mwa mwaka huu.