Ni mwendo wa kusaka pointi tatu kwa Namungo leo

Kikosi chetu leo kitashuka dimbani kuendelea kusaka pointi tatu muhimu wakati tukikutana na Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Majaliwa saa 10 jioni.

Lengo letu mama msimu huu ni kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu na tumejipanga kuhakikisha tunashinda kila mchezo katika mechi zote tisa zilizobaki.

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema mchezo utakuwa mgumu na tutaingia kwa kuiheshimu Namungo lakini matumaini ya kupata pointi tatu ni makubwa.

Matola ameongeza kuwa wachezaji wote 20 waliosafiri na timu wapo kwenye hali nzuri na jana jioni walifanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Majaliwa kabla ya kushuka dimbani jioni ya leo.

“Wachezaji wote waliopo wapo tayari kwa mchezo wa leo, tunajua mchezo utakuwa mgumu. Tunaiheshimu Namungo ni timu bora na inacheza kwao lakini sisi tumejipanga kushinda,” amesema Matola.

TAARIFA YA KIKOSI

Katika mchezo wa leo tutawakosa nyota Clatous Chama aliyebaki Dar es Salaam kutokana na matatizo ya kifamilia, Joash Onyango ambaye bado hajapona vizuri maumivu yake pamoja na Ibrahim anayetumikia adhabu ya kufungia.

MECHI YA KWANZA

Mchezo wa leo ni wa kwanza msimu huu tunakutana kutokana na ushiriki wetu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Namungo walikuwa wanashiriki Kombe la Shirikisho Afrika hivyo tutakutana tena jijini Dar es Salaam Julai kwenye mechi ya marudiano.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Ni mechi ngumu,Ni mechi ambayo hatutakiwi kupoteza nafasi,Chama hayupo ila naamini tuna quality players watakaoifanya kazi yake ipasavyo

    Kila la heri Wanajeshi wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER