Ni mechi ya maamuzi kwa Mkapa leo

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Wydad Casablanca katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utakuwa ni wamaamuzi.

Tunahitaji kupata ushindi katika mchezo wa leo ili kufufua matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwakuwa tutafikisha pointi tano.

Pamoja na kuhitaji kucheza soka safi kwa ajili ya kuburudisha mashabiki lengo kubwa katika mchezo wa leo ni kuhakikisha tunapata pointi tatu.

Benchikha atoa ya moyoni………

Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha amesema hakuna chochote kinachohitajika katika mchezo wa leo zaidi ya ushindi.

Benchikha ameongeza kuwa tunaiheshimu Wydad na tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi katika Uwanja wa nyumbani.

“Kwetu ni mechi ya maamuzi. Tupo kamili kuhakikisha tunapata ushindi na kucheza soka safi, nawaamini wachezaji wangu wapo tayari kuhakisha ushindi unapatikana,” amesema Benchikha.

Zimbwe Jr: Ni fainali kwetu…….

Nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema itakuwa mechi ya fainali kwetu kwakuwa tunahitaji ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu.

“Ni fainali kwetu, tunahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kufanya vizuri, sisi kama wachezaji tupo tayari kupambana hadi mwisho ili kupata ushindi,” amesema Zimbwe Jr.

Ntibazonkiza, Kanoute kuikosa Wydad……

Katika mchezo wa leo tutakosa huduma ya nyota wetu Saido Ntibazonkiza na Sadio Kanoute ambao wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER