Ni mechi ya kisasi leo Kirumba

Leo jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa CCM Kirumba hapa jijini Mwanza kikiwa na kisasi cha kulipiza kwa Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mchezo huu ni wa kisasi kwa sababu kwenye mzunguko wa kwanza, Ruvu Shooting walitufunga bao moja katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Novemba mwaka jana.

Kuelekea mchezo huo, Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema tunatarajia mechi ngumu na tunaiheshimu Ruvu lakini tumejipanga kurejea Dar es Salaam na alama zote tatu.

Matola amesema wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na wapo tayari kwa mchezo huju lengo letu mama msimu huu ni kutetea ubingwa huo wa Ligi Kuu.

“Ruvu Shooting ni timu nzuri na tunakumbuka walitufunga mechi ya kwanza, sisi tupo tayari kwa mchezo na tunahitaji kushinda kila mchezo ili kutetea ubingwa wetu,” amesema Matola.

TAARIFA YA KIKOSI

Nyota wote 21 waliosafiri kuja jijini Mwanza wapo vizuri na morali ipo juu na wanafahamu tunahitaji kushinda ili kulipa kisasi.

Katika mchezo wa leo tutawakosa nyota wanne ambao ni Clatous Chama, Gadiel Michael, Jonas Mkude na Ibrahim Ame kwa sababu tofauti.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER