Ni mechi ya heshima Chamazi Leo

Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Azam Complex kuikabili Azam FC kwenye mchezo wa kuweka heshima wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mchezo huu ni wa kuweka heshima kwa sababu tayari tumeshatwaa ubingwa wa ligi hivyo leo ni kumtafuta mbabe.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza uliopigwa Februari 7, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliisha kwa sare ya mabao 2-2.

Mara zote tunapokutana na Azam mchezo unakuwa mgumu kutokana na ubora wa timu zote ingawa tumekuwa tukipata ushindi mbele yao kama tulivyofanya mara ya mwisho katika mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup mkoani Ruvuma Juni 26.

Kuelekea mchezo huo kocha msaidizi, Seleman Matola amesesema pamoja na kuwa tumefanikiwa kutwaa ubingwa lakini hatutadharau mechi hiyo na tutaingia uwanjani kutafuta pointi tatu.

“Ni kweli tumeshinda ubingwa wa ligi lakini haimaanishi tunazichukulia kawaida mechi zilizobaki. Mechi dhidi ya Azam itakuwa ngumu lakini tupo tayari kupambana kupata ushindi,” amesema Matola.

TAARIFA YA KIKOSI

Katika mchezo wa leo tutakosa huduma ya nyota wanne Bernard Morrison, Jonas Mkude, Miraji Athumani na Ibrahim Ajibu kwa sababu tofauti.

Morrison ameenda nchini kwao Ghana, Mkude suala lake la nidhamu bado halijamalizika, Miraji amepata majeruhi mazoezini

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER