Ni Ama Zao Ama Zetu, Do Or Die Season 2

Kuelekea mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa Jumamosi, Mei 22 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa tumekuja na kauli mbiu ‘Ama Zao Ama Zetu, Do or Die Season 2’ ili kuongeza hamasa kwa wachezaji na mashabiki wetu.

Tumekuja na kauli mbiu hii ili kukumbushana kila mmoja wetu tunahitaji kutinga nusu fainali ya michuano hiyo hivyo tuna kazi kubwa ya kufanya ili kufanikisha jambo hilo.

Tunaingia kwenye mchezo huu tukifahamu tuna kazi kubwa ya kupindua matokeo ya mabao 4-0 ili kujihakikishia nafasi ya kuingia nusu fainali.

Msemaji wa Klabu, Haji Manara amesema Jumamosi tuna nafasi kubwa ya kuweka rekodi barani Afrika ya kupindua matokeo kama wachezaji wetu watajituma kwa asilimia 100.

Manara amesema kwenye mpira kila kitu kinawezekana ukizingatia ubora wa kikosi chetu tunaweza kuwafunga Kaizer zaidi ya mabao matano na kutinga nusu fainali ingawa haitakuwa kazi rahisi.

“Sio kama tunawadharau Kaizer bali sisi ni timu kubwa na bora lakini itawezekana kama wachezaji watajituma kwa asilimia 100.

“Simba hatuhitaji kujitahidi, tunatakiwa kushinda na kupindua matokeo ili kutinga nusu fainali. Hata kama tutawaahidi wachezaji mabilioni ya fedha kama wasipojituma itakuwa kazi bure hivyo wanajua wana kazi kubwa ya kifanya nasi tupo nyuma yao,” amesema Manara.

Viingilio vya mchezo itakuwa kama ifuatavyo:

Platinum Sh 150,000
VIP A Sh 40,000
VIP B na C Sh 25000
Mzunguko Sh 5000.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. Kila kitu kinawezekana katika Mpira,kikubwa wachezaji wetu wasifanye makosa Kama yalopita
    Na viongozi wasiwape pressure wachezaji Wala benchi la ufundi,wawaache wacheze Kama wanavyochezaga ,hii mechi inahitaji utulivu Sana kuliko kuwa na mambo mengi, inshallah tutashinda na kusonga mbele

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER