Ngoma, Lakred wang’ara Kombe la Muungano

Nyota wetu wawili kiungo mkabaji Fabrice Ngoma na mlinda mlango Ayoub Lakred wameng’ara katika michuano ya Kombe la Muungano iliyomalizika Visiwani Zanzibar.

Ngoma ameibuka mchezaji bora wa michuano hiyo wakati Lakred akiibuka mlinda mlango bora wa michuano hiyo.

Ngoma amekuwa katika kiwango bora ambapo hata katika mchezo uliopita dhidi ya KVZ alikuwa mchezaji bora wa mechi.

Kwa upande wake Lakred hajaruhusu bao lolote katika mechi zote mbili huku akicheza dakika 180.

Katika mchezo wa fainali kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza ameibuka mchezaji bora wa mechi (Man of the Match).

Na kwa ubingwa huu tumekabidhiwa kitika cha pesa taslimu Shilingi milioni 50.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER