Uongozi wa Klabu ya Simba, umeweka wazi viingilio vya kilele cha Wiki ya Tamasha la Simba Day ambalo litafanyika Septemba 19 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu, Ezekiel Kamwaga amevitaja viingilio kuwa mzunguko ni Sh 5,000, VIP B na C Sh 20,000, VIP A, Sh 30,000 na Platinum Sh 200,000.
Kamwaga amesema tiketi za Simba Day zimeanza kuuzwa leo na baadaye vitatangazwa vituo ambavyo zitakuwa zinapatikana kupitia mitandao yetu ya kijamii.
"Tumeamua kutaja viingilio mapema wiki mbili kabla ya Tamasha ili kuwapa Wanasimba nafasi ya kukata mapema na kupunguza usumbufu.
"Tunajua watu wengi wamejipanga kujitokeza kwa wingi kilele cha Simba Day kwa hiyo tumepanga viingilio na zoezi la tiketi mapema ili kutoa nafasi kwa watu wengi," amesema Kimwaga.