Kamati ya Uchaguzi ya klabu imetoa ratiba nzima za Uchaguzi ambao umepangwa kufanyika Januari 3.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Anderson David Msumba amesema Katiba ya Simba inataka kufanyika Uchaguzi kila baada ya miaka minne na Uongozi ulio madarakani unamaliza muda wake.
Nafasi zinazoshindaniwa na Mwenyekiti nafasi moja Wajumbe watano ambapo mmoja kati yao lazima awe mawanamke.
Sifa za mgombea kwa upande wa Mwenyekiti lazima awe na elimu ya Shahada wakati Wajumbe wanatakiwa kuwa cheti cha kidato cha nne.
Umri wa mgombea unatakiwa kuanzia miaka 25 mpaka 65 nakuwa mwanachama hai kwa kipindi cha kuanzia miaka mitano.
Hii hapa ratiba kamili ya Uchaguzi
30/10 - 6/11/2026 - Kutoa na kuchukua fomu
7-11/11/2026 - Kurudisha fomu
12-14/11/2026 - Kupitisha na kukagua fomu kwa ajili ya kuzihakiki na Kutangaza majina ya waliokidhi vigezo.
15/11/2026 - Kutangaza majina ya waliokidhi vigezo na kukaribisha mapingamizi.
17-18/11/2026 Kupokea mapingamizi
19-21/11/2026 Kupokea mapingamizi
23-25/11/2026 Kusikiliza mapingamizi
26-27/11/2026 Kutoa maamuzi ya mapingamizi kuhusu wagombea.
30/11/2026 Kutangaza majina ya waliokidhi vigezo vya kugombea.
3/12/2026 - 2/1/2027 Kampeni
3/1/2027 - Uchaguzi